< Malengo Saccoss

Jinsi ya Kujiunga

Sifa za mwanachama

Awe mwenye umri usiopungua miaka kumi na nane (18)

Awe mwenye tabia nzuri, mwaminifu na akili timamu

Awe amelipa Kiingilio, hisa na kuweka Akiba kwa kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa Masharti haya na awe tayari kushiriki kikamilifu shughuli za Chama zinazompasa

Awe tayari kufuata Masharti ya Chama, Sheria ya Vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013 na Kanuni zake wakati wowote

Taratibu za kujiunga

Maombi ya mwanachama yatafanywa kwa maandishi kwa Bodi ya Chama ambayo itayajadili na akikubaliwa atathibitishwa na Mkutano Mkuu

Maombi yakipokelewa ndani ya siku thelathini Bodi iwe imeshughulikia ombi/maombi na kutoa jibu kwa mwombaji au waombaji

Mwanachama atalipa kiingilio cha shilingi laki moja tu (100,000/=) na angalau Hisa tano au zaidi kati ya Hisa Hamsini (50) zenye thamani ya shilingi elfu Kumi (10,000/=) kila moja anazotakiwa kununua ndani ya miezi kumi na mbili tangu kujiunga na Chama

Kuchangia Akiba yake ya shilingi elfu Hamsini (50,000/=) au zaidi kila mwezi

Chama kitakuwa na daftari ya wanachama lenye maelezo muhimu ya kila mwanachama ambapo mwanachama ataweka saini yake